Bull Condom FAQs

Maswali na majibu kuhusu Bull condom

Bull Condom ni nini?

Bull Condom ni mipira ya kiume (Condom) inayovaliwa kwenye viungo vya siri
vya mwanaume (UUME) wakati wa tendo la ndoa (KUJAMIIANA)

Je Bull Condom zinatoka wapi?

Bull Condom zinasambazwa nchini Tanzania na kampuni ya DKT international.

Je Bull Condom zinapatikana wapi?

Bull Condom zinapatikana kwenye maduka ya kawaida na maduka ya dawa kwa shilingi mia tano (500) pekee nchi nzima.

Je kuna umuhimu wowote wa kutumia Bull Condom?

Ndio, kuna umuhimu sana kutumia Bull Condom kwa kila tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu, Bull Condom huzuia magonjwa ya zinaa, mimba zisizotarajiwa na virusi vya Ukimwi. Pia Bull Condom zina humsaidia mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni.

Je vipi kama mwenzi wangu tumepima na tunaaminiana? Kuna haja ya kutumia Bull Condom?

Ndio, ni vyema kutumia Bull Condom wakati wote kwani pamoja na kuzuia magonjwa ya zinaa, mimba zisizotarajiwa na virusi vya Ukimwi. Pia Bull Condom zina humsaidia mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni.

Sijui kutumia Bull Condom, je nifanyaje?

Ili kupata faida hasa za Bull Condom, fuata hatua hizi.

  1. Fungua Bull Condom kwa uangalifu, kucha zako zinaweza kutoboa Condom.Minya chuchu ya Condom, kisha valisha kwenye uume uliosimama.Kunjua Condom kuanzia kwenye kichwa cha uume hadi kwenye shina.
  2. Baada ya kufanya mapenzi, shika Condom kwenye kwenye shina la uume ili isichomoke na uivue kabla ya uume kulala.
  3. Viringisha Condom iliyotumika katika karatasi ya chooni au karatasi nyingine na utupe mahali ambapo watoto hawawezi kuifikia.
  4. Unaweza kutupa Condom iliyotumika kwenye choo cha shimo, si cha kukaa au cha kuflashi. Zingatia hili.
Je naweza kutumia Condom mata ngapi?

Tumia Condom moja kwa tendo moja la ndoa (bao moja). Kwenye kila boksi dogo la Bull linalouzwa shilingi mia tano (500), kuna pakti tatu za Bull Condom. Usifue wala Usivae tena Condom iliyotumika. Tumia Condom MOJA kwa kila tendo.